Rais Donald Trump amemshambulia msaidizi wake wa zamani wa Ikulu ya White house Steve Bannon,kwamba alipoteza akili zake mara tu alipopoteza ajira yake.Trump amefikia hatua hiyo kufuatia Bannon kunukuliwa na kitabu kipya kilichopishwa akiwa anaelezea jinsi mtoto wa rais Trump alivyokutana kwa siri na kundi la watu kutoka Urusi ili kupanga njama za uchaguzi.
Ndani ya kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael Wolff,afisa huyo wa zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo Donald Trump mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi zilizolenga kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze kushinda.
Hata hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu hicho zilizopewa uzito na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white house,rais Donald Trump amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye binafsi na urais wake pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa huyo hakupoteza kazi yake tu lakini alipoteza akili zake pia.
Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim
Trump adai Pakistan imeihadaa Marekani muda mrefu
Marekani yanuia kukata misaada kwa Palestina
''Steve alikuwa ofisa aliyekuwa akifanya kazi kwaajili yangu,mara baada ya mimi kuteuliwa kuwania urais baada ya kuwabwaga wagombea wengine 17,'' amesema Trump.
Amesema pia kuwa Steve anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.
Steve Bannon, ni afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha kazi mwezi August mwaka jana.