SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 10 Januari 2018

T media news

Maskini..Kumbe Tatizo la Wastara Lilianzia Kampeni za CCM

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa tatizo lake ambalo linamsumbua sasa lilianza kipindi cha mwisho wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 za Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuanguka katika kampeni hizo.

Wastara Juma ambaye sasa anahangaika kutafuta milioni 37 kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi nje ya nchi amesema baada ya kuanguka kipindi hicho alisikia maumivu makali sana kwenye mguu wake lakini aliona kawaida ila anadai maumivu ya mgongo ndiyo yalianza kumtisha.

Hata hivyo Wastara amekiri kuwa alipokwenda kufanyiwa matibabu kwa mara ya kwanza alipata 'Support' kubwa kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kwa sasa ameshindwa kwenda kumuomba tena Makamu wa Rais kwa kuwa anahisi awali huenda alikuwa anatumia fedha zake hivyo anaogopa kumpa mzigo mkubwa ndiyo maana ameomba kwa kila mwenye kujua matatizo aweze kumsadia ili akapate matibabu tena.