SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 4 Januari 2018

T media news

Matonnya Aliyepata Msamaha wa Magufuli Naye Ataka Kwenda Ikulu

Wakati Babu Seya na mwanaye wakiwa tayari wametimiza azima yao ya kumuona Rais, Mganga Matonya, aliyeepushwa kifungo cha maisha, analalamikia hali yake kuwa imemzuia kusafiri kwenda Ikulu kumueleza jambo Rais John Magufuli.

Matonya, ambaye alikuwa mfungwa mwenye umri mkubwa kuliko wote kati ya walioachiwa huru, alikuwa anatumikia kifungo cha maisha baada ya awali kupata msamaha wa adhabu ya kunyongwa kutokana na kupatikana na hatia ya kuua na ameishi gerezani miaka 43.

“Mtakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kati ya tuliotoka gerezani niliyetamka kutaka nimuone Rais, lakini hadi sasa nashindwa kumuona,” alisema Matonya ambaye aliiambia Mwananchi siku alipotoka kuwa ana neno la kumueleza Rais na asipopata nafasi, atakufa nalo.

“Siko tayari kumwambia mtu mwingine zaidi ya Magufuli kipenzi changu,” alisema.

Akizungumza kwa simu kutoka Kijiji cha Wiliko, Matonya alisema taarifa za wanamuziki hao alizipata kutoka kwa mtoto wake na kwamba zilimliza kwani angepata nafasi hiyo kabla hajafa, angejisikia huru katika nafsi yake.

“Alipokuja (Rais Magufuli) kwenye mkutano wa CCM Dodoma niliwaomba watoto wangu wanipeleke. Tatizo wanaona kama nimechanganyikiwa lakini siyo kweli,” alisema Matonya.

Mzee huyo aliomba taasisi na mashirika mengine kumsaidia kumuona Rais Magufuli.

Mtoto wake, Aron alisema aandike ujumbe wake hata magazetini na Rais atauona.