Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameunga mkono maamuzi yaliyofanywa na wanachama wa Simba SC huku akisema kuwa watakao kumbukwa zaidi ni wale waliyopinga mabadiliko hayo.
“Leo sina maneno mengi ya kuzungumza nimeshazungumza katika mkutano uliyopita ambao ulikuwa muhimu zaidi yakufikia hapa tulipofika leo.”
“Mafanikio haya hayakuja bure tunatambua uongozi umefanya kazi kubwa sana lakini pia wanachama wamefanya kazi kubwa na wale wasio kubaliana na haya wamefanya kazi kubwa sana.”