SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 12 Septemba 2017

T media news

UCL: Mourinho ataweza kuutafuna mfupa wa Basel uliomshinda Ferguson?

Baada ya miaka miwili Hatimaye Manchester United usiku wa leo wanarejea tena katika usiku wa ulaya, wakifuzu kupitia mlango wa ubingwa wa UEFA Europa League, Leo usiku wimbo wa Champions League utasikika katika spika ya Old Trafford kwa mara nyingine tena.

Manchester United FC leo wanawakaribisha FC Basel 1893, ambao wamekuwa wakiwapa shida saba katika michezo ya huko nyuma.

• United walifuzu kucheza UCL msimu huu kwa kushinda Europa League, ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miaka 22 kushindwa kufuzu kupitia kumaliza nafasi za juu kwenye ligi.

• Mabingwa wa mara 3 wa Champions League wapo kwenye kundi A na wanahitaji kufungua kampeni yao kwa ushindi dhidi ya Basel ambao wameshindwa kuwafunga mara mbili huko nyuma katika uwanja wa Old trafford .

Mechi zilizopita


• Timu hizi zilikutana mara ya kwanza msimu wa 2002/03 katika hatua ya makundi, United wakishinda mechi ya kwanza 3-1 iliyofanyika Switzerland
Ruud Van Nisterlrooy akiweka kambani goli mbili usiku huo. Ole Gunnar Solskjær alifunga goli la 3.

• Giménez alifunga goli la kufutia machozi, na mchezo wa pili walipoenda OT, Gimenez akafunga tena kwenye mchezo uliopigwa March 2003, goli lake lilisaidia Basel kupata matokeo ya sare ya 1-1.


• Basel walipata pointi nyingine muhimu katika dimba la Trafford katika hatua ya makundi msimu wa 2011/12. Magoli mawili kutoka kwa Dabny Welbeck yaliwapa United uongozi kabla ya Fabian Frei (58) na Alexander Frei kufunga mawili (61, 76pen) yaliwapa Nafasi ya kukaribia kushinda mchezo huo kabla ya Ashley Young kusawazisha dakika za mwisho na kuwapa United pointi 1.


• Timu zilizocheza katika mchezo uliopigwa Old Trafford mnamo 27 September 2011 zilikuwa:

United: De Gea, Fábio (Nani 69), Jones, Ferdinand, Evra, Valencia, Anderson (Berbatov 82), Carrick, Giggs (Park 61), Young, Welbeck.

Basel: Sommer, Park, Dragović, Cabral, Steinhöfer, Zoua, G Xhaka, Abraham, F Frei (Chipperfield 77), Streller (Pak 81), A Frei (T Xhaka 89).

Rekodi za Timu • Manchester United walishacheza mechi moja ya ulaya msimu huu, walipofungwa na Real Madrid 2-1 katika mchezo wa Super Cup. Kipigo hicho kilihitimisha rekodi ya United kutopoteza mechi 11 katika michuano ya ulaya (W8 D3) tangu walipofungwa na Fenerbahçe SK katika mchezo wa 4 wa makundi ya Europa League.

• Hii ni mara ya 21 kwa United kushiriki katika hatua ya makundi ya UEFA Champions League , ni mara 4 tu walishindwa kuvuka kwenda hatua iliyofuatia baada ya makundi.

• United hawajapoteza mchezo katika mechi 18 za ulaya zilizopita ambazo walicheza katika uwanja wao wa nyumbani, wameshinda 14 na sare 4, mara ya mwisho kupoteza nyumbani ilikuwa msimu wa 2012/13 katika mtoano dhidi ya Real Madrid.

• Mpaka United imekutana na Basel mara 4 – hizo ndio mechi pekee ambazo United inecheza dhidi ya timu kutoka Uswiss.


Basel • Basel wamefuzu kwa kushinda mara 8 mfululizo ubingwa wa Uswiss.

• Hii ni mara yao ya 8 wanashiriki katika hatua ya makundi ya mashindano haya, msimu uliopita waliishia nafasi ya 4 katika kundi A, wakipata pointi 2 katika mechi 6.