Mkurunzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola ametaja mmiliki wa vichwa vya treni utata vilivyobainika kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.
Baada ya Wizara ya ujenzi na Mawasiliano kusesema haina taarifa ya Vichwa vya treni ambavyo vipo bandarini, rais akaagiza vyombo vya usalama kufuatilia baada ya ununuzi wake kuwa na utata.
Leo Azam TV walimhoji Mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na Rushwa Nchini Valentino Mlowola, amesema Walibaini mchakato wa kununua hivyo Vichwa ulishaanza mwaka 2014/15, lakini hawakufika mwisho na hapakuwa na mkataba wuliosainiwa wa hivyo vichwa kufika nchini au kununuliwa nchini. Shirika linalohusika na Usafirishaji wa reli, ulishaanza mchakato wa ununuzi wa hivyo vichwa hivyo lakini hapakuwa na mkataba wa vichwa hivyo. Ameongeza mmliki wa hivyo vichwa ni Electro-Motive Diesel ya nchini Marekani ndo alivileta hapa nchi lakini hakuna Mkataba wa Mauziano kati ya hiyo kampuni la TRL
Amesema huu uchunguzi kuna vitu viwili vinatoka, unaweza kukuta utaratibu wa kiutawala zilikiukwa au makosa ya jinao yalitendwa. Bado tunaliangalia sababu watuhumiwa wote wameshahojiwa na vielelezo vyote tunavyo. Na kama kuna hatua za kujinai tutapeleka jalada letu kwa mwendesha mashitaka wa Serikali. VIDEO: