Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Rungwe anashikiliwa na Polisi kwa siku ya nne sasa.
Kamanda Mambo alisema kuwa Rungwe anashukiliwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka lakini hakwenda kiundani zaidi kueleza ni nyaraka gani ambazo Rungwe ameghushi kwa kile alichosema kuwa hana taarifa za kutosha.
Hashim Rungwe alikuwa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.