SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 5 Septemba 2017

T media news

Dayna Nyange Afunguka Siri ya Kuingia Kwenye Sanaa ya Muziki

Msanii wa Bongo Flava Dayna Nyange amedai kuwa kipindi cha nyuma muziki wa AY na Fid Q ulimpelekea kupenda muziki na atimaye kutumbikia katika tasnia hiyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’ kipindi cha awali alikuwa akifanya na muziki wa rap kabla ya kuanza kuimba.

“Sasa hivi nikitaka kufanya hicho kitu itanichukua muda sana, lakini mimi nilikuwa napenda kwa uandishi na kuna watu wanaflow, hapo nilikuwa nampenda AY alivyokuwa anaflow lakini kwenye maneno Fid Q ni mtu ambaye alikuwa na maneno,” amesema Dayna.

“Unajua muziki una utofauti unaweza ukawa na maneno makali lakini kwenye flow ukawa na utofauti, mwingine anaflow kiasi kwamba unaleta ladha fulani. Kwa hiyo nikawa napenda maneno ya Fid Q alikuwa na maneno fulani makali na magumu,” ameongeza.