SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 14 Septemba 2017

T media news

Breaking: Mahakama yamuachia huru Yusuf Manji

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 14 imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi yake ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hoja ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake.

Manji ameachiwa huru baada ya kusota rumande kwa miezi kadhaa pamoja na wenzake ambapo walikuwa wakituhumiwa kukutwa na vifaa vya jeshi bila kibali.

Katika kesi hiyo ya msingi ambayo Manji alikuwa na wenzake, walikuwa wakituhumiwa kukutwa na mabalo 43 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya Sh milioni 236.5

Washtakiwa hao pia walidaiwa kukutwa na mihuri ya JWTZ iliyoandikwa “Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ” na “Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma” kinyume na sheria.