SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 14 Septemba 2017

T media news

Matibabu ya Tundu Lissu Milioni 10 Kwa SIku Chadema Yaomba Msaada Jumuiya ya Kimataifa

Chadema imetangaza kuanzisha kampeni maalumu kuchangisha fedha kwa ajili ya kumgharimia mbunge wake, Tundu Lissu anayeendelea kupata matibabu mjini Nairobi huku matibabu yake yakigharimu Sh 10 milioni kwa siku.

Kutokana na ukubwa wa gharama hizo chama hicho tayari kimeziomba jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU) kuangalia kama inaweza kusaidia matibabu ya mwanasiasa huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari amesema leo Ijumaa kuwa pamoja na gharama za kumtibu Lissu kuwa kubwa lakini chama kitaendelea kumpigania ili kuokoa maisha yake.

“Unajua chama tumepoteza watu wengi sana, kama vile Ben Saanani, Dk Slaa ( Willbroad) lakini tuna mahaba makubwa na ndugu yetu Lissu hivyo tunaendelea kupigania maisha yake. Gharama  anazotumiwa kutibiwa ni kubwa mno maana kwa siku inagharimu kiasi cha Sh10 milioni sasa sisi peke yetu hatuwezi ndiyo maana tumeamua kuomba msaada toka kwa rafiki zetu,” amesema.

Amesema chama kimeunda kamati maalumu ambayo inaratibu michango ya Lissu na moja ya eneo ambalo wamewasilisha maombi yao ni kwa Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya.

“Siwezi kusema hadi sasa nini tumejibiwa ila ninachojua kamati inaendelea kufuatilia... unajua wale Wajerumani ni ndugu zetu maana chama cha CDU ni marafiki zetu na tumewaandikia,” amakati wa kubeba uchumi wa taifa