Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka 6 jela au kulipa faini ya Tsh 35 milioni kila mmoja baada ya kuwatia hatia waliokuwa viongozi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Aidhabu hiyo imetolewa leo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha, Elisaph Mathew.
Mbali na adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ameamuru vigogo hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari 26 ambayo ni chakavu kwa gharama ya zaidi ya Tsh 300 milioni.
Katika kesi ya msingi, Mataka alipandishwa kizimbani akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi, tuhuma ambazo zilihusisha ubadhirifu wa fedha zilizotumika kununua magari chakavu.
Katika hatua nyingine, mahakama imemuachia huru William Haji ambaye alikuwa ni Mkaguzi Mkuu wa hesabu za ndani za ATCL.