SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 1 Septemba 2017

T media news

Bombadier ije ianze Kufanya Daladala ili Tulipe Deni la Watu Pole Pole- Rungwe

Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameibuka na kumtetea Tundu Lissu kwa kile alichofanya kutoa taarifa juu ya ndege ya Tanzania kuwekwa kizuizini Canada na kusema ametumia haki yake ya kikatiba ya kutoa habari kuhusu sakata hilo.

Rungwe amezidi kuwashangaa watu ambao wanasema Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa alitoa taarifa hiyo na kusema uzalendo siyo kuficha  au kufanya siri ya mambo yanayohusu maisha ya Watanzania na kudai ni bora watu wajue ili mwisho wa siku hata maisha yanapokuwa magumu wajue kuwa zile fedha za Umma zimechukuliwa kwenda kulipa deni hivyo watu wafunge mkanda.

Aidha Rungwe ameitaka serikali kufanya mazungumzo na watu hao japo waweze kuwapunguzia au hata kama kulipa kwa awamu ili mwisho wa siku ndege hiyo iweze kuja Tanzania na kuanza kufanya safari zake.

"Kesi ile imefikia katika hatua ya mwisho kabisa ya utekelezaji, wanasheria wana mbinu nyingi wanaweza kufanya jambo wale watu ambao ni wadai wakaelewa angalau kutupunguzia tukapata kanafuu fulani au tukalipa hata kwa awamu ni nafuu ndege yetu ikaja ikaanza kufanya daladala yake hapa na kupeleka watu hapa na pale kuokoteza hata hizo senti inaweza kujilipa yenyewe ila ukitumia utemi utemi si kila kitu unaweza kutumia utemi" alisema Rungwe.

 VIDEO: