SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Septemba 2017

T media news

“Acha kelele, saini mkataba” mkongwe wa Arsenal kamjibu Ozil

Juzi Mesut Ozil aliamua kuvunja ukimya juu ya yale yanayoitokea klabu ya Arsenal, pamoja na mengi aliyozungumza lakini Ozil aliwaambia wachezaji wakubwa wa klabu hiyo kwamba waache maneno waiunge mkono timu.

Japokuwa Ozil hakutaja jina moja kwa moja la mchezaji anayesema lakini ni wazi kwamba ujumbe huo uliwaendea Martin Keown, Ian Wright na Thiery Henry ambao mara nyingi ndio wamekuwa wakizungumza sana kuhusu Arsenal.

Sasa Ian Wrigh ameupata ujumbe wa Ozil na ameamua kumjibu kwa kumuambia kwamba aache kujificha katika kivuli cha Alexis Sanchez badala yake kama kweli anaipenda sana klabu ya Arsenal kama anavyodai baasi ashike kalamu asaini mkataba mpya.

“Kama una mapenzi mema na klabu kwanini hujasaini mkataba mpya? Ozil anajificha tu katika kivuli cha Alexis Sanchez kwa kuwa yeye ndio mkataba wake unaongelewa sana lakini bado hajasaini mkataba mpya” alisema Wright.

Wright amesema wachezaji wa klabu hiyo hawajitumi kwa ajili ya kocha wao na ndio maana ahata akishambuliwa kimaneno wenyewe huwa hawajisikii vibaya wanacheza tu watakavyo.

Ian Wright amesisitiza kwamba wao kama wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wana uchungu mkubwa na Arsenal na ndio maana wanaongea mabaya yao ili kuwafanya wajirekebishe na kuwa bora.