SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Septemba 2017

T media news

Jaji David Maraga wa Kenya Ametuonyesha Tofauti Kubwa Kati ya Msomi na Aliye Elimika


Zifuatazo ni sifa za Mtu aliye Elimika
Haogopi
Anajiamini
Hayumbishwi
Kuuwawa Kwake ni sehemu ya Uzalendo wake kwa nchi aliyopo
Ana maamuzi ya mwisho na ya Kishujaa
Msikivu na makini mbele ya Hoja husika
Humtumainia sana Mwenyezi Mungu

Zifuatazo ni sifa za Mtu Msomi
Usomi wake ni wa GPA tu na siyo wa Kiutendaji
Mwepesi Kushawishika
Mnafiki
Muoga sana wa Kufa / Kuuwawa
Huwa si mtulivu na asiyejielewa muda mwingi kuwa anataka nini
Anapenda sana Kujipendekeza na Mfitini
Humkumbuka Mwenyezi Mungu pale tu akiwa na shida au vyuma Kwake vimemkazia

Je na Wewe mwana JF baada ya Jaji David Maraga kutuonyesha kweli maana halisi ya Mtu aliye Elimika unadhani na Wewe hapo ulipo kutokana na hali yako ya Maisha na Utendaji wako hadi kwa Wanasiasa na Viongozi wetu nao wameelimika kama ' Jaji ' au wengi wetu / wengi wao ni Wasomi tu?

Karibuni.