Klabu ya Real Madrid imefuta uteja dhidi ya Barcelona kwa kuichabanga goli 3-1 na kutwaa ubingwa wa kombe la Super Cup nchini Hispania.
Ronaldo akipachika mpira wavuni dakika chache kabla ya kupigwa kadi nyekundu.
Licha ya Mshambuliaji wao tegemezi wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kupata kadi nyekundu kunako dakika ya 82, Madrid walionekana kutokata tamaa na kupambana zaidi.
Goli la kufungua akaunti ya magoli ya Real Madrid lilipatikana kunako dakika ya 60 ya kipindi cha pili baada ya Beki wa Barcelona, Gerard Pique kujifunga kabla ya Ronaldo na Asensio kuonesha viwango vyao na kutupia goli kila mmoja.
Goli la kufuta machozi la Barcelona lilifungwa na Lionel Messi kunako dakika dakika ya 77 kwa njia ya penati baada ya Luis Suarez kuangushwa kwenye eneo la penati, Tazama magoli yote hapa chini