Upinzani nchini Syria watangaza kumuua ndege aliyetumiwa na Israel kufanya shughuli za kijasusi nchini Syria
Upinzani nchini Syria umetangaza kumpiga risasi ndege aina ya Tai aliyekuwa anatumiwa na Israel kufanya ujasusi katika kanda hiyo .
Ndege huyo anasemekana kuonekana maeneo ya Idlib karibu na mpaka wa Uturuki.
Vikosi vya upinzani vilimuua ndege huyo kwa risasi baada ya kugundua kuwa alikuwa anapaa na kuzunguka eneo moja katika kanda hiyo .
Ndege huyo alikuwa amewekwa kamera na vifaa vya uchuguzi katika mwili wake .
Syria imekuwa ikikumbwa na vita kwaa miaka 6 sasa .