Hamu ya tendo la ndoa kwa mwanadamu ni moja ya hisia za msingi kwa mtu wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi.
Pweza ni aina ya samaki ambaye anapendwa na baadhi ya watu hasa supu yake ambayo imekuwa na mkombozi kwa watu wengi haswa wanandoa.
Supu ya Pweza inafaida takribani Tisa mwilini mwa mwanadamu hususani kwa wanandoa na wakinamama wanaonyonyesha ikiwemo virutubisho kuukinga mwili wa mlaji dhidi ya magonjwa kama kansa.
Pweza amejawa virutubishovinavyosaidia kuongeza hamuna kuboresha tendo la ndoa hali inayosaidia mwanamke kuwa katika hali nzuri ya uwanamke wake huku mwanaume kuwa mwanaume wa shoka wakati wa tendo la ndoa
Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.
Ni imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.
Pweza usaidia kusisimua mwili huku wengine wakidai wanatumia kama kiburudisho tu sio kama dawa ya kuongeza nguvu.
Supu hiyo inasaidia sana kwa wanaume kuongeza mbegu na kusukuma hamu ya tendo la ndoa hivyo ufanya wanandoa kuweza kukamilisha jukumu lao la unyumba kwa namna bora zaidi.
na kuongeza heshima kwa wanandoa hao.