SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 14 Agosti 2017

T media news

Je, Uke Wako Unatoa Harufu Mbaya? Hii Ndio Jinsi ya Kumaliza Tatizo Lako

Wanaume wengi kila kukicha huwa wanalalamika kuwa inaboa na inakera kupeana Raha na Utamu na Mwanamke ambae sehemu zake za siri zinanuka. Inawatoa out of the mood, mwisho wake wanaconcetrate kudo fasta, wamalize hamu zao kila mtu aondoke.

Wapo baadhi ya wanawake wanajijua wanasumbuliwa na hili tatizo lakini cha kushangaza hawana muda wa kutafuta solutions za kumaliza tatizo lao (wanaishia kuchekwa kuwa vituko vya mtaa bila kujijua bcoz hawajui kuwa matatizo yao ya uke kutoa harufu mbaya,yanasimuliwa na wale wanaume ambao washawahi kulala nao wakiwa wanapiga story na marafiki zao maskani mtaani).

lakini wapo wanawake wachache wenye busara,ambao wanajijua wanasumbuliwa na hili tatizo na wangependa kujua sababu na jinsi ya kulimaliza,na hao ndio wamenifanya mie niandike hii post
Nitaanza kuelezea sababu kisha nitaelezea ni jinsi gani unaweza kumaliza tatizo lako.

Sababu zinazosababisha uke kutoa harufu mbaya ni kama zifuatazo,

1.BACTERIAL VAGINOSIS
Kwa mujibu wa madaktari bingwa,inasemekana kuwa hili ndio tatizo namba moja linalosababisha uke kutoa harufu mbaya.Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na hili tatizo basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.

Kila uke una bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako,Lakini kama ikitokea hawa Bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ambacho uke wako unaweza kuhimili ndio hapo hiki kitendo kinaitwa Bacterial Vaginosis.

Sababu zinazosababisha Bacterial Vaginosis hazijulikani kwa usahihi lakini madaktari wanasema inaweza ikasababishwa na kitendo cha kupeana Raha na Utamu bila condom especially kama vitu vilivyoingia kwenye uke wako wakati wa kupeana Raha na Utamu vilikuwa vichafu(vitu kama vidole au mashine ya mwanaume,or may b dildo etc) au mara nyingine inatokea naturally bila sababu.

Ukitaka Kujua kuwa unasumbuliwa na Bacterial Vaginosis,utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke kutoa maji maji mazito au mepesi yenye rangi ya njano(yellow) au Brown yenye harufu mbaya
Maumivu kwenye maeneo ya kiuno au nyonga
Unaweza usipate au ukapata maumivu ya kichwa.
Uke wako unaweza ukawa unawashwa au usiwashwe (ur vagina might itch or not)

2. YEAST INFECTION
Hili Pia ni Tatizo,lipo kama la Bacterial Vaginosis.tofauti yake ni kuwa kwenye Bacterial Vaginosis waliokuwa wamezidi ni bacteria lakini huku wanaozidi ni fungus candida albicans. Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacterial Vaginosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast Infection japo mara moja katika maisha yao.

Mara nyingi Yeast Infection hutokea Naturally au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa especially kama vimejaa yeast(vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe etc) Ukitaka kujua kama unasumbuliwa na Yeast Infection,utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke wako ukawa unawashwa au usiwashwe (ur vagina might itch or not) Maumivu kama uke unaungua pale unapokuwa unajisaidia haja ndogo (when u pee) Uke kutoa maji maji mazito yenye rangi nyeupe kama jibini(cottage cheese)

3. SEXUALLY TRANSMITTED DISEASES (STDs)
Kuna baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na kupeana Raha na Utamu bila Condom,kama vile Chlamydia na Gonorrhea(kaswende na kisonono),kama ukiyapata huwa yanasababisha Uke kutoa Harufu mbaya kwa sababu dalili zake zinahusiana na kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya.

4. VAGINAL OR CERVICAL CANCER
Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi(cervical cancer),kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ni sehemu ya dalili zake.Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,kama ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu kama ukiwahi mapema.

5. POOR HYGIENE
Inawezekana pia tatizo la uke wako kunuka linasababishwa na uchafu. May b unaoga mara moja tu kwa siku au siku nyingine hata hauogi. Hauna mazoea ya kufua nguo zako za ndani(underpants),na ikitokea siku umezifua basi hata hauzisugui zikawa safi.n.k

MAMBO UNAYOTAKIWA KUFANYA UKITAKA UKE WAKO USITOE HARUFU MBAYA

1. OSHA UKE WAKO KWA MAJI SAFI KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA HAJA NDOGO(PEE)
Asilimia kubwa ya wanawake hawana mazoea na utaratibu huu.Ni utaratibu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanamke. Unapokuwa unajisaidia haja ndogo,most of the tym lazima utakuwa umechuchumaa/umechutama(umesquat),haja ndogo yako inapokuwa inatoka,lazima kutakuwa na mabaki kidogo kidogo yatakurukia na kubakia kwenye lips za nje au za ndani za uke wako(labia majora or minora).

Hayo mabaki baada ya muda yatachanganyika na jasho(sweat) na kutengeneza harufu mbaya,kwa hiyo ili kujiepusha na yote haya,ni heri ukaosha uke wako kwa maji safi kila ukimaliza kujisaidia haja ndogo.

2. UKIWA UNAOSHA SEHEMU ZAKO ZA SIRI,TUMIA MTINDO(STYLE) WA KUPELEKA MKONO KUTOKA MBELE KURUDI NYUMA
Kuna baadhi ya wanawake teyari wameshazoea kusafisha sehemu zao za siri kwa kupeleka mkono kutoka nyuma kuja mbele.Huu mtindo sio mzuri kiafya kwa kuwa huko nyuma kuna Tigo (anus), na kwenye Tigo kumejaa uchafu na bacteria wengi tu.Sasa wakati unajisafisha,unapopeleka mkono nyuma unakuwa kama unazoa bacteria na uchafu kutoka kwenye Tigo,halafu ukauleta mkono mbele unakuwa unawaacha hao bacteria na uchafu kwenye uke wako. Na huo ndio mwanzo wa uke wako kutoa harufu mbaya na kupata infections za ajabu ajabu.

Ukitaka kuwa salama,haijalishi kuwa umemaliza kujisaidia haja kubwa au ndogo,au wakati unaoga,ukitaka kusafisha sehemu zako za siri,tumia mtindo wa kupeleka mkono mbele kurudi nyuma ili usije kuwaleta bacteria na uchafu wa Tigo mbele.

3. VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA(COTTON)
Pamba(cotton) ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana. Na sehemu za siri za Mwanamke zinahitaji flow ya hewa inayopita,nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako za siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.

Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote,nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.

4. USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA
Kwa jinsi maumbile ya Mwanamke yalivyo,unatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.

May b ulivaa nguo ya ndani asubuhi,ikifika mchana,ingia ladies room(bafuni/chooni),Vua Nguo yako ya Ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima(which is better) au ukasafisha sehemu zako za siri.Nguo ya ndani uliyovua unaweza ukaifua(which is better) au ukaikunjakunja na kuiweka ndani ya kipande cha khanga au kitenge ndio uweke kwenye handbag yako ili kama ikitokea ukaopen handbag yako in public,watu wataona khanga au kitenge,hawatojua ndani umeweka nini.

5. PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI AU YEAST KWA WINGI
Unaweza ukapunguza uwezekano wa kupata Yeast Infection au Bacteral Vaginosis kwa kuacha au kupunguza kula vyakula vyote vyenye sukari au yeast kwa wingi.

Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe/bia n.k
Ukizidisha Vyakula au vinywaji hivi,ina maana utakuwa unazidisha yeast mwilini,na wakizidi kwenye uke utapata yeast Infection,mwisho wake uke wako utaanza kutoa harufu mbaya.

6. BADILI PADS ZAKO MARA KWA MARA UNAPOKUWA KWENYE SIKU ZAKO
Ili kuzuia uke wako usitoe harufu mbaya kipindi ambacho upo kwenye siku zako,inashauriwa kubadili ur pad mara kwa mara(may b after each 4 or 6 or 8 hours,it will depend how many pads can u afford per day) Kubadili pads mara kwa mara kunasaidia ujisikie upo comfortable,inazuia bacteria kujikusanya,inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata infection na mwisho inaondoa uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.

7. NYOA (SHAVE) NYWELE ZAKO ZA SEHEMU ZA SIRI MARA KWA MARA
Nywele zako za sehemu za siri zinapokuwa ndefu,unakuwa umetengeneza maficho(hiding place) ya kila aina ya uchafu kuanzia jasho,majimaji yatakayokuwa yanakutoka ukeni ukiget aroused,mabaki ya haja ndogo n.k Ili kuepusha yote haya ni heri ukawa unazikata nywele zako za sehemu za siri mara kwa mara.

8. NENDA HOSPITALI MAPEMA NA HARAKA TENA SANA
Yaani hata usichelewe,kwani haya matatizo especially Bacteral Vaginosis na Yeast Infection ni matatizo ambayo yanaweza kutibika kwa dawa.Ni heri uwahi mapema ili uongeze uwezekano wa kupona haraka bila matatizo.