SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 21 Julai 2017

T media news

Lukaku aiongoza United kuiua Man City

Alfajiri ya leo kulipigwa moja ya pambano kubwa na maarufu duniani likizihusisha timu jirani na zenye uhasimu kutoka jiji la Manchester nchini Uingereza.

Manchestet Derby ni pambano ambalo popote linapopigwa linakuwa linakuwa linavuta hisiaza watu na leo watu wa Marekani wamefanikiwa kuiona Manchestet Derby.

United wameendeleza wimbi lao la utemi baada ya kuinyuka Man City kwa mabao mawili kwa sifuri huku mabao yote mawili yakifungwa katika kipindi cha kwanza.

Romelu Lukaku ameendelea kupasia nyavu baada ya kufungua ukurasa wa mabao kwa United dakika ya 37 kabla ya Rashford kuongeza lingine dakika ya 39.

Hii ni rekodi nzuri kwa Lukaku kwani kati ya mechi 3 alizocheza amefunga mara 2, huku kikosi cha United kikiwa hakijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi za pre season.