Baada ya kufanya uchunguzi Kamati imebaini kuwa ACACIA haikusajiliwa nchini Tanzania, ACACIA haina sifa ya kupata leseni ya kuchimba wala kufanya biashara ya madini nchini:- Mwenyekiti Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
ACACIA MINING inafanya biashara ya madini kinyume na sheria za nchi, hili jambo ni la ajabu linaweza kufanyika Tanzania tu lakini nchi nyingine haliwezekani - Mwenyekiti Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
Kuna Taasisi za serikali kama TRA wamekuwa wakishirikiana na ACACIA wakati watu hao hawatambuliki kisheria, hili jambo linaweza kutokea Tanzania tu si nchi nyingine - Mwenyekiti Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
Baadhi ya watumishi wa serikali wamelitia aibu Taifa, kwa kutoa taarifa za uongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu - Prof. Nehemiah Osoro. #RipotiYaMchanga
#RipotiYaMchanga