1.Kamati ya wanasheria na wachumi ya kuchunguza mchanga wa madini iliteuliwa Aprili 10 ikiongozwa na Prof. Nehemiah Osoro.
2.Miongoni mwa hadidu za rejea ambazo kamati ilipewa ni kujua idadi ya makotena yaliyosafirishwa nje ya nchi tangu 1998.
3.Kamati pia ilitakiwa kuchunguza kama Tanzania inauwezo wa kutengeneza 'smelter' nchini, gharama zake na muda utakaotumika.
4.Kamati ilitakiwa kuchunguza tofauti ya mapato ambayo Tanzania ilipata na ambayo ilitakiwa kuyapata tangu mwaka 1998.
5.ACACIA inayojinasibu kama mmiliki wa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi haijawahi kuwasilisha nyaraka za umiliki huo.
6. Kamati imebani kwa mujibu wa nyaraka kuwa kampuni ya ACACIA PLC haikusajiliwa nchini
7.Kamati imebaini kuwa wamiliki wa makampuni ya madini nchini wametenda makosa mbalimbali ya jinai.
8.Kamati imeridhia baadhi ya watumishi wa serikali, makampuni ya usafirishaji na TMAA wameliingiza Taifa hasara kwa makusud.
9.Makampuni ya Pangea na Bulyahulu yamepatikana na hatia ya kuliingizia Taifa hasara kwa kutokutoa taarifa sahihi juu ya uzito wa makinikia:.
9.Idadi na uzito wa makontena ya mchanga ulionekana kuwa mkubwa kwenye meli tofauti na kwenye nyaraka za bandarini.
10.Baadhi ya makampuni ya wakala wa meli ziliwasilisha nyaraka za uongo za usafirishaji wa madini kati ya 1998 na 2017.
11.Makontena 30 ya futi 20 yenye makinikia yalionekana kwenye nyaraka yamesafirishwa, lakini ukweli yalisafirishwa 33.
12.Kupitia hati ya usafirishaji wa makontena melini, idadi kubwa ya makontena yalikuwa yakisafirishwa bila kuorodheshwa.
13.Migodi ya Bulyanhulu na Pangea imekuwa ikipata faida lakini faida halisi haikuwa ikionyeshwa.
14.Kamati imebaini makontena 44,277 kwa kiwango cha chini yalisafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 na 2017.
15.Viwango vya dhahabu kwa kila kontena ni 28kg, kwa miaka yote ni tani 1,240 kwa kiwango cha chini, thamani yake Tsh 108tril
16.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 ni trilioni 132.56 kwa kiwango cha chini.
17.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 ni trilioni 229.9 kwa kiwango cha juu.
18.Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58
19.Kodi ya Mapato ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 ni trilioni 55 katika usafirishaji wa makinikia.
20.Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 ni bilioni 94 katika usafirishaji wa makinikia.
21.Mh Rais jumla ya Kodi tulizopoteza ni Sawa na makadirio ya bajeti ya serikali kwa kiwango cha Mwaka 2017/18 kwa miaka 2.
22.Taarifa ambazo zimekuwa sikiwasilishwa TMAA kuhusu uchenjuaji wa makinikia hazina ukweli wowote.