Ripoti ya kamati ya pili kuhusu mchanga wa madini imewaibua Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Sengerema, Wiliam Ngeleja kuhusu mikataba ya madini iliyoingiwa miaka iliyopita.
Mbali na hao pia imewaibua marehemu Dk Abdallah Kigoda aliyekuwa Mbunge wa Handeni na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Majina ya viongozi hao yameibuka leo wakati mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Nehemiah Osoro alipokuwa akiwasilisha matokeo ya ripoti yake.