Umoja Wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( Uvccm ) umemtaka aliyekuwa waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya chadema Edward Lowassa kufuta fikra ya kuwa Chadema itaibwaga CCM hata kama kutakuwa na UKAWA.
Kauli hiyo imezungumzwa na kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka na kusema kuwa.
“Kwa bahati mbaya Lowassa amesukumwa na hasira na kujikuta akijitoa CCM mwaka 2015 kama mtu aliyekuwa anacheza ngoma kwa kwenda upinzani huku akiwa na matumaini ya kuukwaa urais.Alisema kama kuna kosa kubwa ambalo Lowassa amelifanya ni kitendo chake cha kuhama CCM na kwenda upinzani hasa Chadema ,Kwa sababu yeye mwenyewe alishawahi kutamka hadharani akihutubia mkutano wa hadhara mwaka 2006 akilinganisha upinzani ni watoto wanaokimbilia mdundiko”.Lowassa asikubali kucheza tombola katika siasa,Siasa ni hesabu na ina formula zake.Nafikiri amekurupuka kujiondoa CCM ameupanda mkenge kwenda Chadema ajue kuwa si Ukawa wala Udeta wenye ubavu wa kuiondoa CCM madarakani alisema Shaka.
Alimtaka Lowassa kujua kuwa hata viongozi na wanachama wa upinzani hawamwafiki mwanasiasa huyo kwa asilimia kubwa,kwani wapo viongozi aliowakuta ambao wametoa jasho jingi kuvijenga vyama vyao hivyo hawapo tayari kumpisha agombee tena urais.
Pia Kaimu katibu mkuu Shaka alifafanua kuhusu kauri iliyotolewa na Lowassa kwa kusema kuwa Tanzania kuna ukandamizwaji wa demokrasia..Shaka alisema
“ Haiba ya demokrasia iliyopo Tanzania huwezi kukutana nayo popote Afrika mashariki,Afrika na duniani kwa ujumla,Ila uamuzi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwahimiza wananchi kufanya kazina kuzalisha mali viwandani na mashambani.Uhuru wa demokrasia au watu kujitawala bila shibe na maendeleo ya kisekta ni upuuzi.
Alisema kwa msisitizo ndugu Shaka.Pia aliendelea kusema kuwa
“Tumemaliza kampeni na uchaguzi mkuu kila mmoja sasa afanya kazi, kukusanya watu kwenye makongamano na kuwapa bahashishi ni kuwapumbaza kiakili ikiwa bado ni Maskini" alimaliza kusema ndugu Shaka..
Source
Gazeti la Mtanzania la mei 15,2017 toleo Na.8546
Ukurasa wa 8.