SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 3 Mei 2017

T media news

MRISHO Mpoto Awacharukia Wanaomsema Vibaya kwa Kumuunga Mkono Rais Magufuli..!!!


Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amedai kuwa amekuwa akitukanwa matusi pamoja na kutupiwa maneno ya kejeli tangu aonyeshe nia yake ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

Msanii huyo ambaye huwa anafanya sho nyingi za Ikulu, amesema yeye ataendelea kumuunga mkono Rais huyo kwa kuwa ni kiongozi ambaye anawapigania wananchi wa chini.

“Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA” lakini kumtukana mtu mwingine sio busara hata kidogo, kwa kuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia,” ameandika Mpoto kupitia mtandao wa Instagram.

“Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa nilioyasema. Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo,” ameongeza.

Mpoto amedai kuwa imekuwa ni tamaduni kwa baadhi ya watu kuwashambulia watu ambao wameonyesha nia ya kumsapoti Rais Magufuli.

“Kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kunaibuka kundi la wapinga maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI.  Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe,” ameongeza Mpoto.