SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 22 Mei 2017

T media news

IMEFICHUKAA..Hiki Hapa Ndio Chanzo cha Wazazi Waliofiwa na Watoto Wao Ajalini Arusha Kujitoa Kwenye Kamati ya Gambo..!!!


Wazazi waliokuwepo kwenye kamati ya rambirambi ya msiba huo iliyoundwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha wamejitoa rasmi katika kamati hiyo.

Kwa mujibu wa mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake linukuliwe ameeleza Sababu kubwa ya wao kujitoa kwamba ni kitendo cha kutumika nguvu ya dola hasa wakati ambapo kulikuwa na ibada ya kupewa pole na rambirambi , ibada ambayo haikufanyika kutokana na kuvamiwa na Jeshi la Polisi na kukamatwa Meya wa jiji la Arusha mh. Kalisti Lazaro ,Katibu wa TAMONGSCO kanda ya Kaskazini Mh. Leonard Mao , Waandishi wa Habari 10 , pamoja na wamiliki wa shule binafsi waliokuwepo katika hafla hiyo.