Baadhi ya mashabiki wanajiuliza kwanini Barcelona walimuacha Daniel Alves aende Juventus. Kile kinachoonekana ni kwamba alionekana kama vile ameisha kutumika kwenye kikosi cha Barcelona. Lakini Alves anaonyesha uwezo mkubwa ambao unawafanya mashabiki wa Barcelona kumtamani.
Barcelona imekosa ubingwa wa ligi wakati Daniel Alves amekua kwenye kikosi ambacho kimeweka historia ya kuchukua ubingwa mara sita mfululizo. Juventus hadi sasa ina titles za ubingwa 33 kama ukitoa ambayo walivuliwa.
Gianluigi Buffon amekua mchezaji ambaye anaangaliwa kama anamaliza maisha yake ya soka kwa furaha na kushinda titles licha ya kuwa na umri mkubwa.
Daniel Alves ameonyesha uwezo wa kupiga tackles kamili, kufanya maamuzi sahihi kwenye idara ya ulinzi na kuwa mchezaji ambaye anaendelea kuleta impact kwenye timu.