Nimeangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinacharushwa Live na Star TV kila Jumamosi asubuhi. Namshauri Dialo atafute muda kipindi hiki kirudiwe jioni wakati wa prime time ili wengi waone.
Kipindi cha leo kusema ukweli muongozaji Dotto Bulendu na Ansbert Ngurumo wameitendea haki tasnia ya Habari dhidi ya vitisho vilivyotolewa jana na rais Magufuli.
Naomba nisiingie ndani sana kuhumu Ngurumo na Bulendu walisema nini kuhusu rais kutaka kuipangia media nini cha kuandika, mimi najikita kwa watu ambao ni wasaidizi wa rais wanajukumu la kumsaidia.
Haya chini ni yangu.
Tanzania ni nchi yetu sote na sio nchi ya mtu mmoja, japa Tanzania ya sasa ni Tanzania ya Magufuli kama ilivyo Darisalamu ya Makonda.
Rais Magufuli ni kiongozi wetu, ni rais wetu, kutokana na kuwa yeye ndiye rais, taasisi ya urais ndiyo ni mamlaka kuu kiutawala kuliko mamlaka nyingine zote, ila pia Magufuli ni binadamu, sio malaika, hawezi kufanya kila kitu yeye peke yake ndio maana amewekewa wasaidizi mbalimbali wakiwemo washauri.
Kunawakati rais kama rais anatoa matamko tata au maamuzi tata yanayoashiria kuwa rais hakupewa ushauri sahihi kabla, kisha waziri wake anakuja kuibuka baadae na kuirekebisha kauli ya rais kwa kuifuta na kuweka mambo sawa.
Mfano mzuri ni siku ile rais alipotoa tangazo hili
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
kisha waziri wake akaja kuibatilisha kauli hii kwa kusema rais alikuwa anatania tuu watani zake. Rais anapozungumza kwenye hotuba inayotangazwa moja kwa moja kwa taifa zima na akatangaza jambo fulani, hii maana yake ni kulitangazia taifa. Sijadhani kama Watanzania walichagua rais Msukuma ili atoe maagizo kwa watani wake Wazaramo kwenye matangazo ya moja moja mubashara ya kulitangazia taifa zima. Kauli yoyote ya rais ni sheria.
Rais kama binadamu na kama Msukuma ana haki ya kutaniana na watani zake Wazaramo vyovyote vile ataona inafaa, lakini utani huo ama autolee kwa Wazaramo wwnyewe na sio mubashara kwa taifa zima, na utani kama huu ukitolewa kwenye matangazo mubashara ya moja kwa moja kwa taifa zima, then rais akiishatoa utani kama huo amalizie kwa kusisitiza ni utani tuu au kwa Wazaramo tuu.
Kuna vitu rais wetu anasema au anafanya vinavyoashiria amekosa ushauri sahihi.
Mfano mzuri ni issue ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, hii issue imekuwa too much mishandled hadi kumchafulia rais na kumjengea chuki ndio maana kwenye mitandao ya kijamii watu wamekasirika sana hadi kumkosea heshima na kutoa lugha za machukizo.
Japo mimi sio mtu wa serikali, bali naamini Wakuu wa Utumishi wa Umma wote popote walipo ni wasaidizi wa rais. Wasaidizi wa rais wanaoaswa kuwa pro active kumsaidia rais wakali wote na sio kusubiri hadi waulizwe rasmi ndipo wasaidie.
Kadhia ya Paul Makonda kutumia vyeti ya kughushi na kufanya udanganyifu ilipoibuka tuu, kabla haijafikia stage ya kumchafulia rais, wasaidizi wa rais wanaohusika walipaswa kujitokeza wao na kumweleza rais ukweli kuwa ni kweli Paul Makonda ndie Daud Albert Bashite na yote yanayosemwa kumhusu mtu huyu ni ukweli kabisa hivyo wangemshauri the right thing to do, hili jambo lingekuwa limekwisha, lakini kumfukuza Waziri Nape kwa hasira na kuendelea kunyamaza as if nothing has happened, hukuwezi kusaidia kitu kuondoa hizo negative perception. Solution ya kudumu ni kuja na ukweli tuu. He has to tell the truth and the truth will set him free. Nikimaanisha baada ya ukweli kujulikana kuwa Daud Albert Bashite ndiye Paul Christian Makonda, then kwa wanaoujua ukweli huu kuwa Daud Albert Bashite ndiye Paul Christian Makonda, kwao he will always be Daud Albert Bashite, and never will he be Paul Christian Makonda, na huyu Paul Makonda he is an imposter!. Na kwa wale wote wanaomfahamu Paul Christian Makonda as Paul Christian Makonda, wataendelea kumfahamu kama Paul Makonda but with much skepticism and reasonable doubt kuwa could he be the real one or ni imposter hadi tuhuma zile zikanushwe rasmi kuwa ni uongo na uzushi!.
Tukija kwenye tukio la uvamizi wa Clouds Radio, Msaidizi wake Nape did the right thing kwa ku come forward na kusema wazi ule ni unajis wa mtu binafsi na sio serikali. Japo kuunda tume wasn't the right approach Nape kama Msaidizi wa rais ambaye ni Waziri, Makonda ni bwana mdogo sana kwake, angemkabili kuupata ukweli yeye and go straight kwa rais kumpa first hand information na kumwachia rais kufikia uamuzi.
Rais angekuwa ameshauriwa vuzuri na wasaidizi wake wanaoujua damage control, wangemshauri rais kuwa dogo ame mess, hivyo ili kulipa millage ya kutosha tukio la rais wa Benki ya Dunia, rais hakupaswa kusema chochote kumhusu huyo dogo. Tukio la uvamizi wa RC kwenye Chumba cha Habari ni tukio kubwa kuliko hata Benki ya Dunia ingehamishia strong room yake pale ikulu kutokana na proximity na impact ya news ya uvamizi.
Juzi asubuhi rais anafanya uteuzi mpya kwa hasira bila kutengua uteuzi wa zamani, kisha akaenda bandarini kwenye ziara ya kushtukiza. Huku nyuma akatokea kichaa mmoja kumtishia bastola waziri wake aliyetumbuliwa. Kihabari yaani ki newsworthyness, tukio la waziri kutishiwa bastola na kichaa fulani ni bigger news kuliko rais kutembelea bandarini.
Kwa vile rais hakufurahishwa jinsi media haikutoa umuhimu stahiki kwa matukio ya msingi yenye umuhimu mkubwa sana kwa taifa, na yeye pale ikulu anayo kurugenzi yake ya habari, lilikuwa ni jambo dogo tuu hata kuteta na Msigwa kwa kumuuliza hivi hii inakuwaje, Msigwa angemweleza tuu ukweli what was news kuliko rais kuonyesha hasira kwa media.
Wasaidizi wa rais wa kila eneo wana wajibu wa kumsaidia rais wetu kwa kumshauri kufanya uamuzi sahihi na kumwachia rais kufanya uamuzi wowote ila sisi kama Watanzania tuna shauku ya kumuona kila wakali rais wetu akifanya na kutenda the right thing at the right time and doing it right. Handling ya Makonda-Bashite-Nape Thing was a wrong thing, done at at a wrong time and done wrongly!.
Washauri wa rais mko wapi na kumuona rais wetu anasema na kutenda as if hana washauri?! .
Sisi jf tutaendelea kushauri kwa lengo la kujenga.
Tanzania ni yetu sote na rais Magufuli ni rais wetu wote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Jumamosi njema.
Paskali