Muigizaji maarufu wa vichekesho Steve Nyerere amemshauri Mh.Nape Nauye kumshukuru Mungu na kumuomba kwa kutenguliwa uwaziri kwa kuwa hajui ameepushwa na jambo gani.
Akiongea na eNewz Steve Nyerere ameendelea kusema kwamba Mh. Nape nje ya uwaziri alikuwa ni msanii pia na alikuwa anaithamini thamani ya msanii na kuilinda pia alikuwa akipenda maendeleo ya wasanii na maendeleo yake na alikuwa na uwezo wa kupiga simu hata usiku kufuatilia masuala ya sanaa.
Amemshauri Nape aendelee kuwa karibu na wasanii na kuwashauri kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya sanaa nchini.
"Nape kama waziri aliyekuwepo, ajue kuwa ana jukumu la kuwashauri wasanii kupiga hatua, kuondoka kwake siyo kuwakimbia wasanii, abaki kuwa mshauri wa wasanii kupiga hatua na kusonga mbele.. Nape ana uwezo mkubwa sana, ana ushawishi mkubwa sana" Amesema Steve
Hata hivyo Steve alimalizia kwa kumshauri Nape kukaa na familia yake na kusali kwa kuwa Mungu ndiye alipanga apewe madaraka ya kuwasimamia wasanii lakini pia amshukuru kwa kuchukua cheo hicho kwa kuwa hajui Mungu kamuepusha na nini na asiogopeshwe na miguno ya wananchi"
Steve pia amemsihi Dkt. Mwakyembe kukabiliana na changamoto lukuki zinazoikabili sanaa