SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 25 Machi 2017

T media news

Muswada wa bima ya afya wa Trump wakataliwa

Muswada wa bima ya afya wa Donald trump wakataliwa bungeni

Rais wa Marekani Donald Trump amewalaumu wapinzani wake wa cham cha Democrats kwa kushindwa kuidhinishwa kwa mpango wake wa afya.

Mabunge yote mawili yanadhibitiwa na wanachama wa Republican lakini muswada huo uliondolewa siku ya Ijumaa kwa sababu ulishindwa kupata kura ulizohitaji.

Akizungumza na gazeti la washington Post, Trump alisema ''hatukuweza kupata kura hata moja kutoka kwa wanachama wa Democrat na tukaona haya hivyobasi kuondoa muswada huo''.

Kuondolewa kwa muswada huo katika dakika za mwisho ni pigo kubwa kwa rais.

Hatua ya kuuondoa muswada huo wa Obamacare ilikuwa mojawapo ya ahadi zake za uchaguzi wakati wa kampeni.

Spika wa bunge Paul Ryan alisema kwamba yeye na bwana Trump walikubaliana kuuondoa muswada huo ,baada ya kubainika hautapata kura 215 za chama cha Republican zilizohitajika.

Chama cha Republican kina wanachama wengi katika mabunge yote mawili ya uwakilishi na Seneti.

Hatahivyo, ripoti zilisema kwamba kati ya wanacha 28 hadi 35 wanapinga sheria hiyo mpya ya afya ya rais Donald Trump.

Wengine walidaiwa kutofurahishwa kwamba muswada huo ulikuwa unapunguza sana bima ya afya huku wengine wakidai kuwa mabadiliko hayo hayatoshi.

Muswada huo pia hakupendelewa na umma huku asilimia 17 pekee ukiuunga mkono.

Trump amesema kuwa amejifunza mengi kufuatia hatua yake ya kutaka kuuondoa muswada huo ikiwa ni miongoni mwa ahadi zake za kampeni ya uchaguzi alizotoa.

Amesema kuwa sasa ataangazia marekebisho ya kulipa kodi.

Kiongozi wa chama cha Democrat Nancy Pelosi amesema kuwa ni ushindi wa raia wa Marekani.Trump alikiri kwamba mabadiliko ya bima hiyo ya afya yaliofanywa na mtangulizi wake Barrack Obama yatasalia kutekelezwa kufuatia kushindwa kwa chama cha Republican kuuondoa OBamacare.