Nadhani Mhe.Rais hajui maana ya uzalendo. Na pengine anadhani kwa kuwa Rais basi yeye ni Mzalendo kuliko wote. Ni mtazamo potofu. Kuwa Rais wa nchi au ngazi yoyote ya UONGOZI na madaraka katika taifa letu, sio kigezo cha uzalendo , japo inategemewa hivyo,
1. Kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia vyama vya siasa visifanye mikutano ya hadhara , huo sio uzalendo.
2. Kutisha vyombo vya habari visitangaze askari anyetoa bastola hadharani kinyume na taalume na maadili yake , huo sio uzalendo.
3. Kukemea na kufokea wahanga wa tetemeko la ardhi kwa kudai setikali haikuleta Tetemeko huo sio uzalendo.
4. Kutumia vyeti amabavyo sio vyako , huo sio uzalendo.
5. Kuvamia vituo vya Tv za watu kwa maslahi yako binafsi , huo sio uzalendo,
Msigwa the MP For iringa urban 24/3/2017