SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 25 Machi 2017

T media news

Msukuma - Sioni Tatizo kwa Mhe Nape Kuonyeshwa Bastola,Mbona Mimi Nilionyeshwa SMG Nane na Sikulalamika,Pia Aaache Kulilia kwa Kutenguliwa Kila Mtu Anauhitaji Uwaziri..!!!!


Akihojiwa Jana, Msukuma alidai kwa walichokifanya watu wanaodaiwa ni askari kumuonyesha bastola mhe Nape ni sahihi kwani kitambulisho cha askari yeyote ni bastola au bunduki hivyo Nape hakupaswa kuwa na shaka maana walikuwa wanamlinda. Msukuma alienda mbali zaidi na kusema hata yeye alionyeshwa SMG nane lakini hakuwa na shaka maana wale ni askari.

Aidha Msukuma Alisema Kuwa Mhe Nape Alipaswa Kutulia kwanza hata kwa miezi mitatau ndipo angezungumza aliyotaka kuzungumza.

Pia Amemsihi Mhe Nape Kuacha Hasira  mara baada ya kutenguliwa kuwa Waziri kwani wakati anaomba kura katika jimbo lake la Mtama aliomba hakuomba na uwaziri ,hivyo asilie kuenguliwa katika wazifa huo kwani bunge lina wabunge 360 na kila mbunge angependa kuwa waziri,hivyo kuenguliwa kwake katika nafasi hiyo inawapa nafasi wabunge wengine nao kuwa mawaziri siku moja na hata yeye anatamani kuwa waziri