Mbeya City wamaliza mchezo, kazi kwenu Yanga
KLABU ya Simba imeng’ang’aniwa na Mbeya City huku ikilazimishwa sare kutoka sare ya bao 2-2, katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mbeya City ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Nchimbi baada ya Raphael Alpha kuuacha mpira nyuma na yeye kuuwahi.
Hadi mapumziko, Mbeya City walikuwa wakiongoza kwa bao 1 huku Simba wakiwa hawajapta kitu. Kipindi cha pili Simba walirudi na ari mpya huku wakishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kusawadhisha kunako dakika ya 65 kupitia kwa Ibrahim Ajib mara baada ya kuchonga mkwaju mzuri wa adhabu.
Mchezo ukawa wa kushambuliana kwa zamu huku Simba wakiongeza nguvu zaidi. Dakika ya 79 Kenny Ally akaiandikia Mbeya City bao la 2 kabla ya Simba kusawadhisha tena kunako dakika ya 85 baada ya kichuya kucheza mkwaju mkali wa penati baada ya Zimbwe kuagushwa na Kabanda na kupigwa kadi ya njano.
Simba wanazidi kuongoza kwa pointi 55 na mabao ya kufunga 40 huku mbele ya Yanga wenye pointi 52 na mabao 49 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Sasa Ligi imenoga, sasa kazi kwao Yanga kuhakikisha wanashinda mechi zijazo ili kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.