Rapa Young Killer amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli alikuwa ‘Inspired’ kuingia kwenye muziki na msanii Dogo Janja kwani yeye alikuwa anaamini ili msanii aweze kufanikiwa na kutoba kwenye muziki ni lazima awe na umri fulani.
Young Killer alisema hayo jana baada ya kukutanishwa live yeye pamoja na Dogo Janja kwenye kipindi cha FNL ndipo alipokiri kuwa baada ya kuona Dogo Janja ametoboa na kuwa mkubwa ndiyo yeye akaongeza nguvu za mitikasi mpka na yeye akatoka kimuziki.
Dogo Janja & Young KIller
“Mimi napendaga kusema ukweli kipindi nahangaika na mishe zangu nilikuwa naamini ili utoboe kwenye muziki ni lazima uwe na umri fulani, sawa Young D alikuwepo na alipata nafasi tukawa tunamuona kwenye matangazo ya show na nini lakini nilikuwa sijaamini kama katoboa.
“Au anaweza kufanya kama tunavyofanya sasa lakini Janjaro alipokuja kutoka ndiyo nikaamini kabisa kumbe unaweza kutoboa ukiwa na hali yoyote muda huo huo na mimi nikaanza kujipanga nikapata mashavu kwa hiyo alikuwa Inspiration kwangu” alisema Young Killer.