Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.
Hitmaker wa ngoma ya “Hakuna Matata” Country Boy ameamua kutazama upande wa pili wa biashara tofauti na muziki ikiwa ni katika suala zima la kujitafutia kipato
Country Boy
Ikiwa muziki ni biashara ambayo inakwenda na wakati, mkali huyo ameamua kuitazama kwa jicho hilo ili kujiwekea misingi mizuri katika kujipatia kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Yawezekana ndoto za baadhi ya wasanii wengi ni kumiliki migahawa ya Chakula lakini huenda kinachosumbua ikawa ni mitaji au namna ya kuanza biashara hiyo rasmi.
Country Boy ameingia kwenye list ya Wasanii wa Bongo walioamua kuwekeza muda wao katika kutoa huduma ya Chakula na huduma hiyo ameipa jina la Country fast food delivery ambayo kazi yake ni kusambaza chakula kwa yoyote anaehitaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Country Boy alipost ujumbe huu..
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Inshaallah kesho Tunaanza Country Fast Food Delivery Msosi Heavy Kwaajili Yako Chenye Upishi Mzuri Na Smart Mapishi Ya Kinyumbani Kabisaa”.