SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Februari 2017

T media news

Tenaaa..Mfumo Mpya wa Kutumia Namba za Simbu Kuanzishwa Mwezi Ujao,Utaruhusu Kuhama Mtandao Mmjoa Kwenda Mwingine Bila Kununua Laini Mpya..!!!


Mfumo mpya wa matumizi ya namba za simu (Number Portability) unatarajiwa kuanzishwa ifikapo Machi Mosi kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za simu nchini.

Kampuni za simu zilizoingia katika mkataba huo ni pamoja na Tigo, Vodacom, Airtel, TTCL, Zantel, Smile, Smart na Halotel.

Jana, TCRA ilitangaza huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa simu nchini, itakayomwezesha mteja kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine na kuendelea kutumia namba yake ya awali.

Mpango huo tayari umeshatekelezwa kwenye nchi nyingi za Ulaya na hata Afrika Kusini.

Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi, Musa Aziz amesema pamoja na faida zilizopo bado kuna hofu kwa watumiaji kutokana na usumbufu wa mawasiliano.

“Nafikiri kutakuwa na gharama za ziada mimi nikimpigia mwenzangu sitajua kwa wakati huo anatumia mtandao gani, hapo ninaweza kuingia gharama kubwa zaidi, sina hakika kama italeta unafuu japokuwa ni mpango mzuri,” amesema Aziz.