KURUGENZI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta,’ Asha Baraka hivi karibuni aliruka skendo ya wa wanamuziki wake kutumia madawa ya kulevya kwa sasa ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli wameapa kuiangamiza biashara hiyo.
Madansa wa Twanga Pepeta
Akizungumza na gazeti hili, Asha alikiri kuwa awali baadhi ya wanamuziki wake walikuwa wakitumia madawa hayo hali iliyompa wakati mgumu na kulazimika kuwapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanzishwa nyumba za kuwatibu (Sober Houses) kipindi hicho. Wewe si unamjua … (anamtaja aliyewahi kuwa mnenguaji maarufu kisha anamtaja na aliyewahi kuwa rapa tegemezi wa bendi hiyo) wale mimi nilikuwa nikiwafungia ndani kwangu ili wasionane na wauza ‘unga’ lakini baadaye nikagundua kuwa walikuwa wakiwapenyezea sehemu fulani kwa siri.
Asha Baraka
Nilipobaini hivyo niliwapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo walikuwa chini ya uangalizi. Unajua niliingia gharama kubwa maana niliwapeleka kule VIP ili wapate matibabu mazuri maana hali zao zilishakuwa mbaya na walikuwa wakishindwa hata kutimiza majukumu yao ya kikazi,” alisema Asha na kuunga mkono vita hiyo iliyoanzishwa na Paul Makonda.