SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Februari 2017

T media news

Producer Mr T Touch Aingilia Kati Bifu ya Young Killer na Young Dee

Producer Mr .T Touch kutoka Studio za Touchez Sound ameingilia kati bifu ya Marapa wawili Young Killer na Young Dee baada ya Marapa hao kuzinguana juzi walipokutana kwenye studio zake maeneo ya Sinza.

Sasa leo Producer Mr T Touch ameingilia Bifu hilo kwa kuwapa ushauri wasanii hao wawili kuwa wasiendekeze bifu za maneno na kutishiana kupigana badala yake waingie Studio na kushindana kwa mashairi na kutengeneza mkwanja.

“Huu ni muda wa Young Killer na Young Dee kutengeneza pesa kwa kufanya collabo sio bifu za maneno na ndiyo maana nimejitolea kuwatengenezea wimbo wao wa pamoja” Amesema Mr T Touch kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.