SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 20 Februari 2017

T media news

Noma Sanaa..Uhaba wa Madawa ya Kulevya Mitaani Wapelekea Mateja Kuhamia Kwenye Ugoro..!!!!



VITA ya kupambana na dawa za kulevya ikiwa imeshika kasi nchini na kusababisha kupungua kwa mihadarati sokoni baada ya wafanyabiashara hiyo kuhofia kukamatwa, watumiaji 'mateja' wameibuka na vilevi mbadala.

Uchunguzi  umegundua kuwa 'mateja' ambao bado wapo mitaani baada ya watumiaji wengi kuonekana kukimbilia katika nyumba za matibabu, wamelazimika kutumia vileo mbadala ili kukidhi haja ya miili yao.

Uchunguzi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambayo huwapo watumiaji wengi wa dawa za kulevya, umebaini kuwa 'mateja' wamehamia kwenye vileo kama mafuta ya petrol, ugoro na gundi ya viatu baada ya kukosa dawa za kulevya.

Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini ambayo imepata msukumo mpya tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ataje watu 65 waliotakiwa kuisaidia polisi kuhusu biashara ya mihadarati wiki mbili zilizopita, ilipata nguvu zaidi wiki iliyopita kutoka kwa IGP, Ernest Mangu.