Mmiliki wa Villa Park Makambako afariki kwa ajali mbaya akiwa na mpenzi wake
Mmiliki wa kiota cha Villa Park cha mjini Makambako, Kizito, amepoteza maisha kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea Jumapili usiku.
Gari ya Kizito baada ya kupata ajali
Ajali hiyo inadaiwa kutokea Morogoro. Inasemekana alikuwa na mpenzi wake ambaye kutokana na mwili wake kusagika vibaya alishindwa kufahamika mara moja.
Kizito alikuwa akitoka kwenye mechi ya mpira kati ya Njombe na Kurugenzi na ajali ilitokea saa nane usiku.
Kizito enzi za uhai wake akiwa amesimama pembeni ya gari yake Toyota Harrier iliyopata ajali