Ney True Boy
STAA wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘ Nay wa Mitego’, anamuonea huruma Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutokana na unafiki unaoonyeshwa na marafiki wanaomzunguka Nay aliiambia Risasi Vibes kuwa kwa masaibu yaliyomkumba mrembo huyo, alitegemea watu wake wa karibu ndiyo wangekuwa wa kwanza kumsaIdia, lakini badala yake wamekuwa wasaliti, wakimpa pole na wakati huo huo wakimchoma kisirisiri.
Wema Sepetu na mama yake
“Anachotakiwa kuelewa Wema ni nani rafiki mwaminifu kwake, asiridhike na marafiki zake wote, ni vema akatambua katika maisha hakuna adui wala rafiki wa kudumu, marafiki huja katika maisha kwa nyakati ambazo wao wanakuhitaji, namuonea huruma kwa kutotambua falsafa hiyo,” alisema Nay.