SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 17 Februari 2017

T media news

NAHREEL ANYOOSHA MAELEZO KILICHOMFANYA APAGAWE KWA AIKA, ATAJA HIKI HAPA

Msanii na mtayarishaji wa muziki wa The industry, Nahreel amefunguka sababu kubwa iliyomfanya kumpenda mpenzi wake Aika, ambaye wanaunda naye kundi la Navy Kenzo.

Nahreel alidai watu wengi wanadhani huenda alimpenda Aika kutokana na uzuri wake wa sura, uzuri wa umbo au uzuri wa kifua chake. Ila ukweli ni kwamba ni kutokana na uzuri wa mashavu yake na siyo hips wala kifua kizuri.


Nahreel & Aika

“Watu wengi wanadhani nimempenda Aika kutokana na umbo lake au kifua chake hapana, kikubwa kilichofanya nimepende Aika ni yale mashavu yake na nimekuwa namtania sana hata usiku napolala huwa nayapiga piga sana, hicho ndicho kilinifanya nimpende Aika” alisema Nahreel alipokuwa akiongea na EATV.