Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. Makonda juzi alifanya operation ya kukamata Watuhumiwa wa uuzaji na utumuaji wa Madawa ya Kulevya, na leo amemtaka Msanii Vanessa Mdee kujitokeza kujibu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya. Operation hiyo ambayo pia imekamata Askari Polisi zaidi ya 10 bado inaendelea ikisimamiwa na yeye mwenyewe RC Makonda.