Wasomi wengi wanapoangalia suala la akili kuna vitu wanasahau. kuwa kuna multiple intelligence. or variety of intelligence. unaweza ukawa na akili ya darasani au akili ya uwanjani ikiwa umchezaji wa mchezo flan.
Michael Jackson alikuwa na akili ambayo wakati mwingine watu wanaamua kuita kipaji. ukiangalia music aliokuwa akiimba na kucheza michael jackson utagundua kuwa alikuwa anatumia akili nyingi sana kuuandaa na kufaham aucheze vipi. Angalia namna ambavyo majukwaa yake yalikuwa yanaandaliwa. wakati flan mpaka kifaru kilikuwa kinaletwa jukwaani.
Angalia tamasha alilolifanya live huko munich ujeruman. wajeruman maelfu walifurika jukwaani wengi wao hata english hawakuwa wakiijua lakini waliimba naye, wengine walizimia kwa hisia, walilia kwa kusikiliza tu maneno ambayo hawakuwa wakijua maana yake. lakini namna alivyokuwa akicheza na kuonesha hisia zake kwenye maneno hayo nao pia walikuwa wakijihisi wanaelewa na kusikia ile hali aliyokuwa akiisikia.
Hii ni kutokana na utunzi wa kiakili na uimbaji pia. utaona pia katika tamasha hilo jinsi ambavyo aliandaa mpaka kifaru kuja jukwaani na mazingira mbalimbali katika wimbo wake wa "What about us"
Akili si walikuwa nazo akina Aristotle,Socrates,Archimedes, Einstein etc. tukiangalia kwa upande huu mwingine pia ni akili nyingi zilitumika kwa yeye kuweza kuteka nyoyo za watu namna ile. kama ni mtu mwenye kuamini ushirikina ungesema aliwaroga ndio maana alipendwa kila sehemu.
Sikiliza mashairi ya nyimbo zake. kama huna akili huwezi tunga mashairi yale. angalia video zake. ambazo pia zilikuwa na maelekezo yake mengi anataka video iweje. Hii yote ni akili. wadau tunapowaza suala la akili tusiangalie upande mmoja tukasahau kila mtu ana akili zake kwa eneo lake.
Aina yake ya uchezaji ambayo ilikuwa ni ya kimapinduzi ni uvumbuzi alioufanya ukiangalia ile style ya moon walker au angalia ule ubunifu wa kwenye wimbo wa smooth criminal pale inapoonekana ameweza kuishinda gravitational force.
Anaenda mwili mzima yeye na wachezaj wake na kurudi pasipo kuanguka. umejiuliza aulitumia mbinu gani? Huoni kama hiyo ni akili kwa lolote alilolifanya?
Tumkumbuke kama mmoja ya watu waliokuwa na akili na wenye mchango wa kipekee hapa duniani. Kwa kupitia music wake wengi walikuwa motivated kuimba na kucheza na wengi waliburudishwa na kuelimishwa.