Kila kukicha mtandao wa Instagram unazidi kuboresha huduma zake ili kuendana na matakwa ya watumiaji kwani tumeona mabadiliko ya huduma za matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya video, ‘InstaLive’.Japo inaonekana kuwa ya kawaida lakini ina utofauti mkubwa na huduma ya mitandao mingine kwa kuwa unapomaliza kuweka matangazo yako hupotea kabisa. Hiyo inamaanisha huwezi tena kusambaza link ya video yako kwa wanaotazama na hawataweza kuiona tena baada ya video hiyo kupotea.
Good news nikwamba, Instagram wapo mbioni kuleta mabadiliko mengine ya kuposti picha nyingi kwa muda mmoja tofauti na mfumo wa sasa hivi wa kuposti picha moja moja.
Kwa watumiaji wa Facebook na WhatsApp ni rahisi sana kuposti picha nyingi kwa wakati mmoja lakini kama unatumia mtandao wa Instagram itakulazimu kuposti picha moja moja hata kama una picha nyingi za kuposti kwa muda huo.
Ila kwa ujio huo Instagram itakuwa imerahisisha kwa watu ambao hupenda kuweka picha za matukio kama harusi au tamasha kwani watakuwa na uwezo wa kuweka picha nyingi kwa wakati mmoja.
Hata hivyo Instagram hawajataja tarehe rasmi ya kuzindua huduma hiyo ingawaje wame sema ni mwaka huu kwahiyo endelea kutufuatilia kwani tutakujuza hapa hapa tukishapata taarifa zaidi juu ya ujio huo.
Source: The Next web