Inawezekana unajiuliza maswali mengi sana kwa nini Simba inapendelea kwenda kuweka kambi Unguja hususan ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Yanga halafu ukawa hupati majibu ya moja kwa moja.
shaffihdauda.co.tz kupitia kwa mwandishi wake Abubakar Khatib ‘Kisandu’ wa Zanzibar imepiga story na mratibu wa kikosi cha Simba kutaka kujua kwa nini inapokaribia mechi ya Simba na Yanga wao hukimbilia kisiwani Unguja kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo huo?
“Nyumbani ni nyumbani, imekuwa kama desturi yetu kuja Zanzibar kwa sababu tunaona tupo nyumbani, kwanza hali ya hewa ni rafiki na tumeizoea halafu kuna vitendea kazi vile ambavyo sisi tunaamini vinapatikana kwa wakati na sisi kuvitumia kwa maandalizi kwa mchezo unaotukabili.”
Simba inaendelea kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan huku wakitarajia kurudi Dar siku ya Ijumaa February 24, tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga Jumamosi February 25, 2017.
Wakati Simba wakikita kambi yao Unguja, mahasimu wao wamekuwa wakielekea kisiwa cha Pemba kufanya maandalizi yao.