SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 2 Februari 2017

T media news

Jinsi ya Kutengeneza Tabia Moja Ambayo ni Muhimu Kwenye Mafanikio.

Mafanikio yana siri kubwa na hutegemeana na mambo mengi, pia kama wengi wanavyosema bahati nayo huusishwa na inasehemu yake katika mafanikio japo wanamaendeleo wengi husema mipango ndo huchangia zaidi, nimeumiza sana kichwa hivi karibuni na kufanya utafiti mkubwa na kuweza kupata jambo moja ambalo ndiyo nguzo kuu ya mafanikio, jambo ambalo hata kama umepewa bahati ya mtende bila hilo jambo kufanikiwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu, jambo ambalo hufanya mipango kukamilika na kutoa matumaini pale mambo yanapoenda kombo.
Kitu kimoja ambacho ni msingi wa mafanikio hua ni Ung'ang'anizi, ung'ang'anizi ni uwezo wa kuendelea kufanya kitu hata kama matarajio ni hafifu kuwezesha kuwezekanika hicho kitu kutendeka, nadhani wote tumeshawahi kuona watu wenye vipaji vizuri sana, watu wenye uelewa mkubwa na watu waliofundishwa kwa hali ya juu wakashindwa kutimiza ndoto zao kwa kukata tamaa mapema, wakakosa ung'ang'anizi wa kufanya mambo yao kuweza kufikia malengo yanayohitajika.

Kwenye maisha mambo magumu ya kukufanya uchanganyikiwe na kutokujua nini cha kufanya siku zote huwa hayakosekania, yasipo kufika leo kesho yatakubishia hodi, ila hakuna kitu kinachoweza kukupeleka kule utakako kama hautokua na ung'ang'anizi wa kufanya mambo na kutokukata tamaa mapema hasa pale unapojiona umeshindwa kabisa, ung'ang'anizi unakufanya urudie kile kitu ulichokishindwa mwanzoni na kukufanya ufanye vizuri zaidi kwa wakati huu, ung'angizi unakufanya uwe na moyo mahari pa kukata tamaa, ung'ang'anizi unakupa nafasi nyingine ya kufanya mambo mahali ambapo ulishindwa mwanzoni.

Habari nzuri ni kwamba ung'ang'anizi ni kitu ambacho sote tunaweza  kuanza kukifanyia kazi na tukawanacho, ni tendo ambalo tunaweza kuligeuza tabia.

Njia sita za kuongeza ung'ang'anizi katika maisha ni kama zifuatazo.

Weka malengo. Mambo mengi huwa hayaendi iwapo usipoyawekea malengo, lazima uwe na lengo na kile unachofanya ili ujue mwisho wa hicho kitu ni kitu gani unataka uwe umekamilisha, kama ni mfanya biashara lazima ujue mwisho wa mwezi au miezi mitatu unataka uwe na faida kiasi gani, au kama ni mwanamuziki unatakiwa uwe na nyimbo ngapi kwa kipindi gani, malengo hukufanya kuwa king'ang'anizi kwa sababu unajua unachoitaji na ni kwa muda gani unapaswa kukitekeleza.Fikiria mwisho utakavyokuwa. Usifikirie malengo madogo madogo uliojiwekea pekee, fikilia lengo kubwa hasa linalokufanya ufanye unachofanya, ni nini utakachopata mwishoni kama iwapo utang'ang'ania kufanya hicho kitu unachokifanya, iwapo jawabu la mwisho ndilo hasa unalohitaji na ndio tarajio lako basi ni rahisi kuwa king'ang'anizi hata kama mambo yakiwa magumu wakati unatenda mambo ambayo yanayo kupelekea kupata hicho unachokihitaji.Badilisha utendaji kazi wako na weka mipaka ya ufanyaji kazi wako. kama iwapo ukiweka mipango, utahitaji kujua kipimo cha maendeleo yako kutokana na mipango uliojiwekea, ila iwapo ukibadilisha utendaji wako wa kazi kuendana na mipango yako itakufanya ujue nini unafanya na wakati gani unapaswa kukifanya, hii itafanya uimili mikiki mikiki ya hali halisi iwe mbaya au nzuri ya utendaji wako wa kazi na kukufanya uwe king'ang'anizi zaidi, na utapata nguvu zaidi ya kufanya unachotakiwa kukifanya sababu una picha halisi ya malengo na utendaji wako wa kazi ulivyo, weka mipaka ya lini unatakiwa uwe umemaliza kile ulichojipangia ili ufanye mambo kwa wakati na mafanikio zaidi.Tembea na kimbia. Huwezi kuwa makini kwenye ufanyaji wako wa kazi muda wote kama unakimbizana na kazi muda wote, utafanya kazi vizuri iwapo utaifanya kwa kasi na pale unapokuwa umechoka unajaribu kupunguza mwendo na kujiachia kidogo ili usije poteza ile hali ya tamaa ya kutaka kukamilisha kazi, ukienda kwa mwendo wa kukimbia pale unapoweza na kutembea pale unapokuwa umechoka itakufanya uifanye kazi kwa muda mlefu bila kukushinda na kuwa king'ang'anizi kwenye hio kazi na kukupelekea kuimaliza.Ondoa vitu vinavyokutoa katika hali yako ya ufanyaji kazi. Huwezi fanya kitu katika hali ya usahihi kama kuna mambo mengine ambayo yanaingilia utendaji wako wa kazi, akili yako ili iwe na uwezo wa kufanya kitu kwa ung'ang'anizi mpaka mafanikio yafikiwe unatakiwa uwe katika hali ya umakini na kile ambacho unakifanya.Badilisha hali ya unavyojichukulia, hadhi ya wewe ujionavyo. Kitu kikuu na muhimu ambacho kitatufanya tuwe ving'ang'anizi ni kubadilisha hali ambayo tunajiona tunayo, iwapo tukiwa tunajiona kama ni watu ving'ang'anizi, na hali ikawa ngumu na kutufanya tutake kuachana na kile tunachokifanya, tutajihisi kama sisi sio watu wa kushindwa na kitu, hali hii ya kujisikia hivi itatufanya tuendelee nacho na kukifikisha mbali.Ndio, kuna vitu vingine sio vizuri kuwa ving'ang'anizi, ila iwapo vinatugusa hali yetu ya kimaisha na inatubidi tuvifanye ili kutoka hali duni kwenda hali ya mafanikio inabidi tuwe ving'ang'anizi.

Vitu vingine sio kwamba huwa ni vigumu ila tunashindwa kuwa na moyo wa kuendelea kuvifanya, tunakosa hali ya kuwa wang'ang'anizi wa kufanikisha jambo kiasi cha kutufanya kushindwa kufikia malengo yetu vilivyo.