SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Februari 2017

T media news

Jina ‘Chuji’ limetoka huku…

Inawezekana hata wewe ulikuwa unaamini kuwa jina la Chuji limetoka kwenye ukoo wa mchezaji iwa zamani wa Yanga Athuman Idd ‘Chuji’ au ni jina ambalo alipewa na wazazi wake.

Kumbe jina hili halina uhusiano kabisa na ukoo wa nyota huyu aliyenza kupata umaarufu akiwa na timu ya Polisi Dodoma, Chuji ni jina ambalo lilikuja baadae ‘nickname’ alilopewa na wachezaji wenzake na baba yake aliyekuwa anacheza katika timu ya Kurugenzi ya mkoani Dodoma.

Hapa Chuji anaelezea kisa kilichopelekea kuzaliwa kwa jina la Chuji ambalo limekuwa maarufu na watu wengine wakiamini ni jina lake halisi ambalo linatoka kwenye ukoo au alipewa na wazazi wake.

“Chuji sio jina langu halisi ni nickname, lilitokea miaka mingi sana nyuma wakati huo baba yangu alikuwa anacheza timu ya Kurugenzi ya Dodoma kipindi hicho nikuwa bado mdogo sana.”

“Siku ambayo lilizaliwa jina la Chuji, kambini kwao (Kurugenzi) walikuwa wamepika wali na maharage sasa inasemekana mimi nilikuwa sitaki maharage nataka mchuzi, kwahiyo  nilipotaka kusema nataka mchuzi nikashindwa badala yake nikasema ‘chuji’ kwa sababu nilikuwa bado siwezi kuongea vizuri.”

“Kwahiyo kuanzia hapo mimi jina langu likawa ni Chuji, wachezaji wenzake na mzee wakawa wananiita kwa jina la Chuji.”

“Wakati nikiwa bado mdogo nilikuwa nacheza na watu watu, wenyewe goli lao na mimi na goli langu lakini nilikuwa nawafunga. Baada ya hapo nilipokuja kupata akili vizuri mpira nilikuwa siutaki, mzee alikuwa anaambiwa kwamba ‘mwanao mbona anajua mpira’ lakini mzee alikuwa hakubali anasema ‘huyu sio mchezaji’ lakini mzee akiniuliza kama nacheza mpira nilikuwa nakataa .”

“Mpira mimi nilikuwa siutaki kabisa,” alipoulizwa alikuwa anataka kuwa nani badala ya kucheza soka? Chuji hakuwa tayari kusema alikuwa anapenda nini badala yake akasema mambo mengine tuyaache nyuma ya pazia.

“Mimi nilikuwa naenda mazoezini saa 12 jioni watu wanakaribia kumaliza mazoezi, nilikuwa navaa pensi ya jeans chini nimevaa moka lakini vitu nilivyokuwa navifanya kila mtu alikuwa anashangaa.”