SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Februari 2017

T media news

DONALD TRUMP KUFANYA MAZUNGUMZO NA NETANYAHU

Rais wa Marekani, Donald Trump amemkaribisha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House ili wafanye mzungumzo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nchi za Mashariki ya Kati.Mazungumzo ya Trump na Netanyahu yanatajwa kuwa yatazungumzia machafuko yanayotokea Syria, utengenezaji wa nyuklia kwa nchi ya Iran na ugomvi unaoendelea kati ya Islael na Palestina.Netanyahu ambaye kwa sasa anafanyiwa uchunguzi baada ya kuwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya pia mazungumzo hayo yanatarajiwa kumaliza utofauti uliopo kwa sasa kati ya Marekani na Israel na kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa katika utawala wa Rais wa Marekani aliyemaliza muda wake, Barack Obama

Aliyewahi kuwa msaidizi maalum wa Rais Obama, Dennis Ross amesema mazungumzo ya Trump na Netanyahu yanaweza kufanikiwa kwani viongozi wote wawili ni kama wameshasahau yote yaliyopita na sasa wanaangalia mbele kushirikiana kwa maslahi ya mataifa yote mawili.