Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa katika mastaa wa muziki Alikiba ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye.
Diva ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji Heri Muziki, alikuwa host wa show ya Valentine’s Day iliyofanyika Jumatano hii katika ukumbi wa Next Door na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.Akiongea na waandishi kabla ya kwenda kusherehesha show hiyo iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Diva alidai Alikiba ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye.
“Alikiba ndiyo msanii au staa ambaye natakamani kudate naye,” Diva alisema baada ya kuulizwa ni staa gani ambaye anatamani kudate naye. “Sijawahi kutoka naye kimapenzi, pia sasa hivi mimi nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine,”
Mtangazaji huyo alidai yeye wanaume wake wengi wanawapata kupitia kipindi chache la Ala za Roho ambacho uchambua mambo mbalimbali kuhusu mahusiano.