SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 5 Februari 2017

T media news

Ajali yaua watano wakiwemo waandishi wa habari

Watu watano wamefariki dunia baada ya gari waliokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka katika eneo la Mwika Mawanjeni Maarufu kama Bar mpya mkoani Kilimanjaro.

Miongoni mwa waliofariki ni waandishi wawili wa habari mmoja akiwa ni wa gazeti la Habari Leo Bw. Anold Swai na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, na mwingine ni mwadishi wa habari wa kujitegemea.